The House of Favourite Newspapers

Fatma Karume Amshtaki Polisi Aliyemzogoa Mahakamani, Adai Fidia Bil. 1

0
Fatma Karume akizozana na polisi.

 

WAKILI wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania dhdi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam.

 

Katika kesi hiyo, Fatma anahitaji alipwe na Inspekta Mwampondela Sh bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake, kumbugudhi na kumzuia kufanya kazi yake (assault, battery, misfeasance in public office).

Fatma Karume akizungumza na wanahabari.

Fatma amesema Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu hali iliyomsababishia maumivu kwenye mkono wake.

 

“Aliniambia kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani ili amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa shikwa mwili wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho kwa wengine,” amesema Fatma.

Fatma ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja wake ili aweze kupata dhamana.
CHANZO: MTANZANIA

Alichokizungumza Tundu Lissu Baada ya Kuachiwa na Polisi kwa Dhamana

Leave A Reply