The House of Favourite Newspapers

Fei Toto Ahidi Kuendelea Mabao ya Mashuti Nje ya 18 kwa Kila Mpira Utakaojaa Mguuni Kwake

0
Mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’.

 

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameahidi kuendelea kufunga mabao ya mashuti nje ya 18 kwa kila mpira utakaojaa mguuni kwake iwe katika Ligi Kuu Bara au Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya juzi kuifungia timu yake ya Yanga mabao mawili katika mchezo wa ligi dhidi ya Azam uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar na kumalizika kwa sare ya 2-2.

 

Katika mchezo huo, Fei Toto ambaye alitokea benchi na kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Denis Nkane, alifunga mabao hayo yote ya kusawazisha kwa mashuti makali nje ya 18.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ akishangilia na Aziz Ki.

Akizungumza na Spoti Xtra, Fei Toto alisema hakubahatisha kufunga mabao hayo, kwani sio mara yake ya kwanza, huku akiahidi kuendelea kufunga tena na tena kwa kila mpira ataoupata nje ya 18.

 

“Nimetimiza jukumu langu la kuipa matokeo mazuri timu yangu. Nitaendelea kufunga aina hiyo ya mabao kwa kila mpira utakaojaa mguuni iwe ndani au nje ya 18.

 

“Nimefurahi kuifungia timu yangu mabao muhimu ya kusawazisha,” alisema Fei Toto.

STORI NA WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

KUMEKUCHA SIMBA, MGUNDA Awekwa KANDO, WAPINZANI wa YANGA Hawajulikani WALIPO | KROSI DONGO..

Leave A Reply