The House of Favourite Newspapers

Fei Toto Apewa Program Maalum Misri Dhidi ya Uganda

0

KIUNGO wa Yanga na timu ya Taifa, Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amepewa mazoezi maalumu kwa ajili ya kumuongezea fitinesi kuelekea .

Stars leo itakuwa mgeni wa Uganda kwenye Uwanja wa Suez Canal, mjini Ismailia nchini Misri ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Afcon.

Kumbuka Desemba mwaka jana Fei Toto alitangaza kuvunja mkataba wake Yanga na tangu wakati huo hajacheza mechi yoyote ya mashindano zaidi ya kufanya mazoezi binafsi.

Gazeti la Championi ambalo lipo mjini hapa tangu Stars wanafika, lilimshuhudia Fei Toto akifanya mazoezi hayo na kwa mujibu wa kocha wa viungo, amesema kuwa kiungo huyo amekuwa akifanya mazoezi mara mbili zaidi ya wenzake ili kumtengenezea fitinesi kutokana na hali yake ilivyo.

Fei Toto alianza mazoezi hayo maalumu juzi Jumatano hadi jana ili kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Uganda.

Na Saleh Ally, Ismailia

Leave A Reply