The House of Favourite Newspapers

Feza Yaendelea Na Elimu Mtandaoni

0
Mkurugenzi wa shule za Feza Tanzania , Ibrahim Yunus .

Baada ya mashule kufungwa kwa kipindi cha siku 30 na watoto wakiwa nyumbani ili kujikinga na janga la Corona ambalo limeikumba dunia nzima, zoezi la ufundishaji katika shule za Feza bado linaendelea kupitia mtandaoni.

 

Shule za hizo za kimataifa zinaendelea na ufundishaji kwa kufanya mapitio ya masomo ili watoto wasisahau kile walichokisoma katika kipindi hiki ambacho wapo nyumbani.

Akizungumza kuhusu suala hilo Mkurugenzi wa shule za Feza Tanzania, Ibrahim Yunus alisema kuwa: “Tunafahamu hiki ni kipindi kigumu kwa dunia yote. Na sisi kama shule tumepokea agizo la serikali la kufunga shule na pia tunaendelea kutumia tehama ya Google Classroom ili kuwa karibu na watoto na kuwasaidia kufanya mapitio ya masomo yao ili wasisahau walichokisoma.

 

Hasa katika kipindi hiki ambapo watoto wapo nyumbani, kumekuwa na changamoto kubwa kwa wazazi jinsi gani ya kuwafanya watoto wanatumia muda wao kwa faida ya kimakuzi na kujiendeleza. Vipindi vyetu vya mtandaoni vinawasaidia wazazi na walezi kulifikia lengo hili. Lakini pia tunawashukuru wazazi kwasababu wanaonyesha ushirikiano mzuri katika kuwasimamia watoto wao katika elimu hii ya mtandaoni.”

 

Ndugu Ibrahim aliongeza pia, “Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwaasa wazazi na watanzania wote kwa ujumla kuzingatia maangalizo ya kiafya tuliyopewa na Wizara yetu ya Afya ili tuweze kulishinda janga hili la corona na tuwaone watoto wetu wakirudi mashulen wakiwa salama .

Leave A Reply