The House of Favourite Newspapers

Fid Q, AY, Msagasumu Wafunika Dawati Concert

0

DAWATI CONCERT (35)

DAWATI CONCERT (34)

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Fid Q ambaye jana ilikuwa siku yake ya kuzaliwa akiimba baadhi ya ngoma zake na mashabiki waliofurika kuwasapoti wanafunzi wa Handeni kukalia madawati. DAWATI CONCERT (36)

Mashabiki wakiwa wamepagawa na burudani kutoka kwa Fid Q.

Boniphace Ngumije na Gabriel Ng’osha / GPL

WASANII mbalimbali nchini jana wamejitokeza kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Handeni iliyopo mkoani Tanga kwa kufanya makamuziki katika tamasha aliloliandaa kwenye Kiwanja cha Taifa cha Burudani, Dar Live kilichopo Mbagala – Zakhem, Dar kwa ajili ya kuchangia madawati kwa wanafunzi wa wilaya hiyo.

Katika tamasha hilo, muitikio wa watu ulikuwa mkubwa na lilipendezeshwa na wasanii mbalimbali. Walioanza kufanya makamuzi mwanzoni mwa tamasha hilo ni pamoja na Bendi ya La Musica Vijana Classic, Mc wa Dar Live Brighton ‘Dalada’ na wengine wengi.

Baada ya shoo kunoga mashabiki wa Dar Live walifurahia muziki mzuri kutoka kwa Bendi ya Injili ya GWT (Glorious Worship Team), Mfalme wa Muziki wa Uswazi maarufu kama Singeli Msaga Sumu, Sterio, Ben Pol, Linex huku Fid Q, AY, Msami na Barnaba wakikamilisha listi kwa makamuzi ya nguvu.

Baada ya wasanii wote kutoa burudani ya nguvu, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ‘Double G’ aliwashukuru wote waliomuunga mkono na akaomba waendelee kujitolea zaidi kwenye masuala ya kujenga taifa.

DAWATI CONCERT (31) DAWATI CONCERT (32)

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, AY akikamua katika tamasha hilo la kuchangia madawati kwa  wanafunzi wa Handeni.

DAWATI CONCERT (33) AY akikamua sambamba na mwanadada aliyeshindwa kujizuia na kupanda stejini.

DAWATI CONCERT (19)

Muandaaji wa tamasha hilo, Godwin Gondwe akimpongeza AY baada ya kukamua jukwaani.

DAWATI CONCERT (22)

Mfalme wa Muziki wa Singeli, Msaga Sumu akiwarusha mashabiki wa Dar Live.

DAWATI CONCERT (23)

Mashabiki wakienda sambamba na Mfalme wa Muziki wa Singeli, Msaga Sumu.

DAWATI CONCERT (29)

Msanii wa R&B, Ben Pol akiwarusha mashabiki kwa ngoma yake ya Sofia.

DAWATI CONCERT (30)

Ben Pol akikamua ngoma yake ya Moyo Mashine.

DAWATI CONCERT (20) DAWATI CONCERT (21)

Waimbaji wa Injili wanaounda Bendi ya GWT (Glorious Worship Team) wakifanya makamuzi ya nguvu kwenye tamasha hilo.

DAWATI CONCERT (24) DAWATI CONCERT (25)

Mwanamuziki Linex akizikonga nyoyo za mashabiki.

DAWATI CONCERT (26) DAWATI CONCERT (27)

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba akifanya yake kwenye shoo hiyo.

DAWATI CONCERT (28)

Mashabiki wakidata na ngoma za Barnaba.

DAWATI CONCERT (1)

Wasanii wanaounda Bendi ya La Musica Vijana Classic wakifanya yao kwenye shoo ya utangulizi katika tamasha hilo lililoudhuriwa na watu wengi.

DAWATI CONCERT (18)

Msanii wa Bongo Fleva, Msami akicheza na mashabiki wake Dar Live.

Dawati Concert 3

Mc wa Dar Live, Brighton ‘Dalada’ (kulia) ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, akikamua pia katika tamasha hilo.

Leave A Reply