The House of Favourite Newspapers

Imamu, Msaaidizi Wake Wauawa Marekani

1

imamu

Leonard Msigwa/GPL

IMAMU Maulama Akonjee (55) na msaidizi wake Thara Uddin (64) wameuawa kwa kupigwa risasi katika mitaa ya Queens jijini New York nchini Marekani. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, wauaji waliotekeleza mauaji yao walifanya shambulio linaloonekana kupangwa.

waombolezaji (1)

Waombolezaji wakiwa na simanzi baada ya mauaji hayo.

Msemaji wa polisi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema, “Hakuna ushahidi wowote unaoonesha mauaji hayo yametokana na mambo ya imani za dini, na mpaka sasa hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa na polisi bado wanaendelea na uchunguzi.”

waombolezaji (2)

Wananchi wenye asili ya Bangladesh wakiwa na majonzi baada ya vifo hivyo.

Imamu huyo akiwa na msaidizi wake waliuawa wakati wakitoka kwenye msikiti wa al-Furqan Jame baada ya sala ya jana Jumamosi kwenye majira ya saba na nusu mchana (kwa saa za Marekani).

eneo latukio

Eneo walipouawa imamu na msaidizi wake.

Imamu huyo mwenye asili ya Bangladesh alikuwa akihudumu msikitini hapo ambako wengi wa waumini wake ni wale wenye asili ya Bangladesh.

1 Comment
  1. Sozi says

    Innalinllah wainnailayh rajiun,the USA government should find who did this and why?there might be a reasons on this

Leave A Reply