The House of Favourite Newspapers

FIESTA LEO KUNA BONGE LA SAPRAIZ LEADERS

0
Vanessa Mdee akicheza na wacheza shoo wake.

Hatimaye leo ndiyo leo kwenye Viwanja vya Leaders Club pale Kinondoni ambapo kutakuwa na bonge la shoo la Fiesta.

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alisema kwamba shoo ya leo itakuwa na utofauti mkubwa dhidi ya zile zilizopita kwani wasanii wamejiandaa vizuri kutoa shoo baab’kubwa pia kutakuwa na sapraiz ambayo anaamini itawafurahisha mashabiki watakaojitokeza Leaders.

 

 

Ruge alisema licha ya kuwa shoo ya aina yake pia wasanii kabla ya kuanza kufanya makamuzi yao watapata fursa ya kutambulishwa kila mmoja kwa mashabiki kwa mtindo wa kupita jukwaani kisha kwenda kukaa nyuma ya jukwaa kusubiria muda wake wa kukamua.

Jux na Ben Pol wakiimba wimbo wa pamoja.

“Nina uhakika shoo hii itakuwa ya aina yake kwetu, kwani hadi hapa ninapozungumza kwa sasa maandalizi yote yamekamilika na haya yamefanywa na wasanii wenyewe kiasi kwamba shoo ya Jumamosi (leo) itakuwa ya tofauti sana na miaka yote ambayo tumekuwa tukiifanya na kwa maana hiyo ninaweza kusema wazi kwamba yeyote atakaye bahatika kuja hapa atapata shavu la kuona shoo ya kisasa kabisa tofauti na huko nyuma.

Nandy na Maua Sama wakifanya yao.

“Kama kuna mtu anadhani haya ninayosema ni ya kubuni, basi niko tayari kujiweka dhamana endapo mtu ataingia Fiesta na asione burudani ya tofauti na miaka ya nyuma basi mimi niko tayari kutoshiriki kwa chochote katika Fiesta ya mwaka kesho,” alisema Ruge.

 

Msimu huu hakutakuwa na msanii kutoka nje na zaidi wameangalia vipaji vya ndani na baadhi ya mastaa wa hapa nchini watakaopanda jukwaani ni Kundi la Weusi, Chegge, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Ben Pol, Nandy, Fid-Q, Darassa, Rostam (Roma na Stamina), Mr Blue, Barnaba, Maua Sama, Vanessa Mdee, Jux, Madee, Aslay, Baraka the Prince, Dogo Janja na Saida Kalori.

Leave A Reply