The House of Favourite Newspapers

Jokate Amuombea Dua Lulu

0
                 Jokate Mwegelo

MWANAMITINDO Jokate Mwegelo hivi karibuni baada ya kukaa kimya bila kumposti msanii mwenzake Elizabeth Michael ‘Lulu’ wala kuongea lolote kuhusiana na hukumu yake ambapo mastaa kibao walionesha kumuhurumia na kumposti kwa kuweka maneno tofauti tofauti, yeye ameibuka na kusema kuwa anamuombea dua huko alikoenda kwani ndio jambo pekee ambalo anaweza kulifanya.

Elizabeth Michael ‘Lulu’

Akilonga na Risasi Jumamosi, Jokate alisema kuwa yeye anamuombea dua Lulu Mungu amfanyie wepesi huko alikokwenda kwani ndio njia pekee ya kumfariji.

 

Mwanamitindo huyo aliongea hayo baada ya kuulizwa sababu ya yeye kutomposti na maoni yake juu ya hukumu hiyo. “Kikubwa ni kumuombea na mimi namuombea ndicho ninachoweza kusema,” alisema Jokate.

STORI: HAMIDA HASSAN

Leave A Reply