Fiesta Yawapagawisha Wabunge Na Mawaziri Dodoma

 jux-vanesa-001Mwanamuziki Vanessa na Jux wakitumbuiza kwenye tamasha hilo.wabunge-001Baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria tamasha hilo akiwemo Profesa Maji Marefu (wa pili kulia), Venance Mwamoto (wa kwanza kulia) na William Ngeleja (katikati).

img_0697-001Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia na Waziri January Makamba.

weusi-001Kundi la weusi likitumbuiza jukwaani kwenye tamasha hilo lililohudhuriwa na mashabiki wengi.

adam-mchomvu-001Mwanamuziki Adam Mchomvu akitumbuiza mbele ya mashabiki lukuki ndani ya Uwanja wa Jamhuri.

b12-adam-001 belle-9-001Mwanamuziki Belle 9 naye alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo, usiku wa kuamkia leo.darasa-001Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki.darasaaaaaa-001Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki.

fiesta-1-001Baraka The Prince akitumbuiza usiku wa kuamkia leo.fiesta-2-001Sehemu ya umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, usiku wa kuamkia leo. fiesta-4-001Mwanamuziki Jux akionesha madoido ya kucheza na jukwaa na mpenzi wake ambaye pia ni mwanamuziki Vanessa Mdee.img_0321-001  sehemu ya mashabiki ambao walifika mapema uwanjani hapo kushuhudia tamasha hilo.img_0335-001

Mmoja wa mashabiki aliyejishindia moja ya zawadi (T-shirt) kutoka kwa waandaaji wa tamasha hilo.

DODOMA, Usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kulifanyika tamasha la Fiesta ambako mamia wa wakazi wa manispaa ya Dodoma na vitongoji vya jirani walihudhuria onesho hilo wakiwemo pia baadhi ya waheshimiwa wabunge na mawaziri wa serikali ya tano wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mheshimiwa Nape Nnauye.

Baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria tamasha hilo ni pamoja na William Ngeleja, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, Venance Mwamoto pia alikuwepo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Attickson na Waziri January Makamba.

Tamasha hilo lilivunja rekodi baada ya kuhudhuriwa na mashabiki wengi na kuacha historia ndani ya viunga hivyo yalipo makao makuu ya nchi yetu.

Wasanii wote walioshiriki kwenye tamasha hilo walifanya ‘show’ kali iliyowapagawisha mashabiki wao na kufanya tamasha hilo liwe la kipekee.

Imeandaliwa na Leonard Msigwa/GPL.

 


Loading...

Toa comment