The House of Favourite Newspapers

Mwinyi Achangisha Shilingi Bilioni Moja Dar Za Waathirika Kagera

matembezi-ya-hisani-chini-ya-rais-mwinyi-8-001Rais  Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akizungumza jambo baada ya matembezi hayo.

matembezi-ya-hisani-chini-ya-rais-mwinyi-1Baadhi ya wadau wakikabidhi mfano wa hundi ya fedha walizochangia.

matembezi-ya-hisani-chini-ya-rais-mwinyi-2Wadau kutoka makampuni mbalimbali wakiendelea kukabidhi mfano wa hundi kuchangia

matembezi-ya-hisani-chini-ya-rais-mwinyi-4-001Rais  Mstaafu,  Ali Hassan (katikati) akiwaongoza viongozi mbalimbali wa kiserikali na watu wengine katika matembezi hayo ya kilometa tano.

matembezi-ya-hisani-chini-ya-rais-mwinyi-5-001Watu mbalimbali wakimuunga mkono Mzee Mwinyi katika matembezi hayo. matembezi-ya-hisani-chini-ya-rais-mwinyi-7-001Baadhi ya wananchi waliomuunga mkono Mzee Mwinyi wakishikilia mabango yenye ujumbe wa waathirika wa tetemeko.

matembezi-ya-hisani-chini-ya-rais-mwinyi-6-001Bras Bendi ya jeshi la polisi ikiongoza matembezi hayo.

RAIS  Mstaafu wa Awamu ya Pili,  Ali Hassan Mwinyi leo amechangisha zaidi ya  Sh. 1.5 bilioni katika matembezi maalum yaliyofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi,  Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu.

Fedha hizo zimetokana na michango pamoja na ahadi za wadau mbalimbali waliojitokeza kushiriki kwenye matembezi hayo yaliyokuwa yakilenga kuchangia walioathirika na tetemeko na yaliitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa chini ya Waziri Dk Augustine Mahiga.

Matembezi hayo yalikuwa ni ya  kilometa tano. Akizungumza viwanjani hapo baada ya kukamilisha taratibu za uchangiaji wa fedha kwa ajili ya waathirika hao, Mwinyi aliwashukuru wote waliojitokeza na kuchangia zikiwemo taasisi mbalimbali na makampuni binafsi kwa kufanikisha zoezi hilo na kupatikana kiasi cha fedha hizo.

Hata hivyo amewataka kuendelea na moyo huo kila panapotokea maafa kwani alisema yatupasa kushikamana.

PICHA NA STORI: DENIS MTIMA/GPL.

Comments are closed.