The House of Favourite Newspapers

FIFA Yaifungia Yanga Kusajili Kwa Kukiuka Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP)

0


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Yanga Sc ya Tanzania kusajili wachezaji kwa kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebainisha kuwa Young Africans Sc haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

Leave A Reply