The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Saba Wahofiwa kupoteza maisha baada ya gari la Shule kuanguka kwenye korongo Arusha – Video

0

Wanafunzi Saba wanahofiwa kupoteza maisha baada ya gari la Shule ya Msingi Ghati Memorial kuanguka kwenye korongo linalopitisha maji Mitaa ya Dampo, Sinoni

Inadaiwa chanzo ni dereva kushindwa kulidhibiti gari alipofika eneo la tukio kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia usiku hadi alfajiri ya leo Aprili 12, 2024

Taarifa kutoka eneo la tukio imedai kuwa Wanafunzi saba hawajulikani walipo, Watatu wameokolewa na mwili mmoja umepatikana, Dereva wa gari naye ameokolewa na yupo chini ya ulinzi

JamiiForums ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema “Nipo kwenye msafara, ila hizo taarifa nimezipata, kikosi cha Uokozi kipo eneo la tukio na Wanafunzi saba hawajulikani walipo wengine wameokolewa, taarifa kamili tutaitoa baadaye.”

Leave A Reply