The House of Favourite Newspapers

Fiston Aanza Mikwara Yanga SC – Video

0

FISTON Abdulazack, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kusaini mkataba ndani ya timu hiyo ni ukubwa wa timu hiyo.

Fiston raia wa Burundi amemalizana na mabosi wake hao na amesaini dili la miezi sita baada ya kufikia makubaliano mazuri.

 

Mrundi huyo anaungana na kiungo mshambuliaji, Said Ntibanzokiza ambaye tayari ameshaanza kutumika ndani ya kikosi hicho.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Fiston alisema kuwa ukubwa wa Klabu ya Yanga nje na ndiyo umemshawishi yeye kujiunga na timu iyo kwenye msimu huu. “Nimesaini Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na inajulikana nje na ndani ya nchi hivyo nami nimekuja pia kuungana na timu hii.

 

“Najua wengi wanapenda kuona nitafanya nini wasiwe na mashaka nitafanya vizuri na kila kitu kitakuwa sawa, “ alisema Fiston.

 

Yanga ipo nafasi ya kwanza chini Kocha Mkuu, Cedric Kaze ina pointi 44 baada ya kucheza mechi 18 ndani ya Ligi Kuu Bara.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply