The House of Favourite Newspapers

Fiston Afanya Balaa Mazoezini

0

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Fiston Abdoul Razak raia wa Burundi, amefanya balaa la hatari mazoezini katika kujiandaa na mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

 

Yanga ikiwa kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar, juzi Ijumaa ilimpokea nyota huyo aliyetokea kwao Burundi akijiunga na timu hiyo baada ya kukamilisha usajili wa dirisha dogo.

 

Katika usajili wa dirisha dogo, Yanga mbali na kumsajili Fiston, pia imewanasa beki mzawa, Dickson Job na Said Ntibazonkiza raia wa Burundi.

 

Baada ya juzi Ijumaa kuwasili hapa nchini na kutambulishwa, akaingia kambini moja kwa moja, kisha jana Jumamosi akaanza mazoezi na wenzake.

Siku ya kwanza mazoezini, inaelezwa kwamba jamaa huyo alifanya mambo ya hatari ambapo mtu mmoja kutoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo, amelieleza Spoti Xtra ufundi wa Fiston.Mtoa taarifa huyo, alianza kwa kusema:

 

“Fiston amekabidhiwa jezi namba 7 ambayo ilikuwa inavaliwa na Mapinduzi Balama ambaye kwa sasa bado hajatengamaa akiendelea na matibabu.“

Alikuja Ijumaa na kutambulishwa kwa wachezaji, lakini leo (jana Juma-mosi) alianza mazoezi na amekuwa ak-iwashangaza wache-zaji wenzake kwa namna alivyo na uwezo ka-tika umiliki wa mpira na utoaji wa pasi.

 

“Anaonekana kuwa mwepesi na ana maamuzi ya haraka akiwa na mpira jambo ambalo litakuwa na matokeo mazuri kwetu ligi itakapoendelea pamoja na mashindano mengine, hivyo tunasubiri ligi iendelee kijana auwashe moto.”

Spoti Xtra lilimtafuta Meneja wa Yanga, Hafi dh Saleh kuelezea maendeleo ya kambi yao akisema: “Kwa sasa ni wachezaji watatu ambao wanaendelea vizuri na program zao ambao ni Yacouba Songne, Said Ntibanzokiza na Dickson Job.

 

“Wengine ambao hawapo ni wale ambao walikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars (Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa, Feisal Salum na Deus Kaseke). Kuhusu mchezaji Fiston tayari ameanza mazoezi na wenzake.”

 

FISTON AFUNGUKA

 

Akizungumzia namna alivy-opokewa ndani ya Yanga pamoja na mipango yake, Fiston alisema: “Nafurahi kuona nimepokewa na mashabiki wengi sana, kwagu mimi ni jambo geni, hivyo nimeona jinsi gani wana Yanga walivyokuwa na upendo mkubwa kwangu kitu ambacho naamini nina deni kubwa sana kwao.“Hivyo naahidi kuwatumikia vizuri ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mengi nikishirikiana na wachezaji wenzangu ambayo naamini yataifanya timu kuendelea kuongoza ligi ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa msimu huu.

 

”INJINIA HERSI APIGILIA MSUMARI

Akizungumzia mipango yao katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia, Hersi Said, alisema: “Tumekamilisha kwa kiasi kikubwa mipango tuliyokuwa nayo kabla ya kuanza msimu huu, ambapo shabaha yetu kubwa ilikuwa katika maeneo matatu ya utawala bora, idara ya ufundi iliyo thabiti na wachezaji wa kiwango cha juu.

 

“Kazi hiyo tumeikamilisha kupitia usajili bora wa wachezaji na kuajiri makocha wenye viwango, tayari matunda yameanza kuonekana kupitia ubingwa wa mapinduzi na mwenendo mzuri kwenye ligi.“Tunashukuru Mungu katika hilo na wakati huu tumebaki na lengo moja tu la kuhakikisha tunaibuka mabingwa msimu huu.”

WAANDISHI: Joel Thomas, Marco Mzumbe, Lunyamadzo Mlyuka na Ibrahim Mussa

 

WAANDISHI WETU,Dar es Salaam

Leave A Reply