The House of Favourite Newspapers

Fistoni Mayele Aongoza kwa Kupendwa na Wanawake Bongo

0
Fistoni Mayele.

MCHEZAJI mahiri wa Yanga, Fistoni Mayele anaongoza kwa kupendwa na wapenzi wa mpira wa miguu wanawake Bongo.

Utafiti uliofanywa na Ijumaa kwa kuwahoji wanawake 200 jijini Dar es Salaam umeonesha kuwa Mayele alipigiwa kura na wanawake 175 akifuatiwa na Saido Ntibanzokiza ambaye alipata kura 20 huku Moses Phiri akipata kura 5.

Wanawake hao waliulizwa swali moja tu kwamba kati ya wachezaji wa mpira wa miguu nchini, ni mchezaji gani unapenda uchezaji wake.

Licha ya wanawake hao 200 pia na watoto wadogo ambao wengi walionesha kumpenda Mayele na wengi wao walisema wanapenda staili yake ya kushangilia ambayo imeenea karibu nchi nzima.

Stori; MWANDISHI WETU Dar | GPL

SAKATA la MAPATO SIMBA na YANGA LAZUA BALAA BUNGENI – “KWA NINI WAPATE MIL.188 KWENYE MIL . 400?”

Leave A Reply