The House of Favourite Newspapers

Mzozo wa Sudan: Uingereza Yamhamishia Balozi Wake wa Sudan, Ethiopia

0

Uingereza inasema Giles Lever, balozi wake nchini Sudan, amehamishiwa katika nchi jirani ya Ethiopia baada ya kufungwa kwa ubalozi wake kwa muda, kulikosababishwa na mzozo katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

‘’Kutoka Addis Ababa, ataongoza juhudi za kidiplomasia katika kanda hiyo ili kumaliza vita nchini Sudan”, Wizara ya mambo yan je ya uingereza ilisema katika taarifa.

Hadi sasa, Waingereza 536 wamekwisha okolewa kutoka Sudan, mamlaka za Uingereza zimesema.

Lakini kumekuwa na ukosoaji wa kuzorota kwa uokoaji wa serikali ukilinganishwa na nchi nyingine za Magharibi.

Jeshi la Sudan na kikundi cha jeshi la dharura – Rapid Support Forces (RSF) wamekubaliana kuongeza muda wa mkataba wa usitishaji kwa saa nyingine 72 zaidi.

AJALI MBAYA: PRADO LAGONGA LORI PWANI, MPISHI MAARUFU LILIAN CATERING AFARIKI…

Leave A Reply