The House of Favourite Newspapers

Flaviana Matata Atoa Vifaa vya Masomo Shule ya Msinune, Pwani

0

TAASISI ya Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata imetoa vifaa vya masomo ikiwemo mabegi pampja na kalamu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Msata Katika Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani.

Mkurugenzi huyo ambaye aligawa vifaa hivyo kwa wanafunzi wapatao 345 akisindikizwa na Mbunge wa Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata Foundation alisema kuwa , taasisi hiyo ilianza kufanya ukaarabati katika Shule hiyo mwaka 2016 huku akisema kwamba akilinganisha hali ilivyokua awali na sasa ni tofauti kwani Majengo yalikua chakavu tofauti na sasa ambapo wameweza kufanya ukarabati , kuweka miundombinu ya maji na umeme.

Aidha Matata aliongeza kwa kusema kuwa Taasisi hiyo baada ya kumaliza kukarabati majengo hali ambayo imeweka mazingira rafiki kwa wanafunzi, hivi sasa wanajipanga kujenga nyumba za waalimu huku akimuomba Mbunge wa Chalinze kusaidia baadhi ya vifaa vya ujenzi ili kwa pamoja waweze kulifanikisha lengo hilo.

 

Akizungumza kwenye mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa amepokea kwa mikono miwili ombi la ujenzi wa nyymba za Waalimu kwani katika taasisi zetu bado tunachangamoto nyingi lakini kwa kupitia Taasisi ya Flaviana Matata Foundation nina imani wote kwa pamoja tutaunganisha nguvu kwa kutumia mfuko wa Jimbo nyumba hizo za Waalimu tutazijenga.

“Flaviana umetupiga teke kutoka mbali kwani ukirudi miaka 20 nyuma wakazi wa Kijiji hiki cha Msinune hawakuwa na mwamko wa elimu tofauti na ilivyo sasa nakiri hilo” alisema Kikwete huyo.

Alisema kuwa ana anamuomba Mwanamitimdo huyo wa Kimataifa kuwatatulia changamoto ya soko la zao la Mananasi ambapo kwa kupitia Taasisi yako unayo nafasi ya ya kutusaidia karika kututafutia fursa za soko la mananasi nje ya nchi ikiwa ni katika kukuza uchumi wa Chalinze.

 

Kila inapofika mwanzo wa Muhula Taasisi ya Flaviana Matata hupeleka vifaa vya shuleni ,pia kwa kupitia Taasisi hiyo wamekuwa wakitoa udhamini kwa wanafunzi katika Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu nchini.

Wakati huohuo Flaviana Matata ametoa wito kwa wazazi kuacha kuwakatisha watoto wao wa kike masomo na kukimbilia kuwacheza ngoma.

 

“Baba zangu na mama zangu nawaomba sana muachane na tabia ya kuwakatisha masomo mabinti zenu kwani elimu ndiyo ufunguo wa maisha hivyo wakati umefika sasa wa kuachana na mila potofu ambazo zinapoteza matumaini ya njozi zao katika maisha yao ya baadaye wao wakiweza kusoma watakuja kuwa msaada mkubwa sana kwenu na kwa jamii nzima kwa ujumla.

Leave A Reply