The House of Favourite Newspapers

Flora Mvungi Atoboa Siri za Tanzanite!

0
Flora Mvungi.

TANZANITE ni mtoto wa mastaa wawili Bongo, waigizaji ambao pia ni wanamuziki, Hamis Baba ‘H-Baba’ na Flora Mvungi.

Mbali na Tanzanite, wawili hawa wana mtoto mwingine wa kiume aitwaye Afrika.

Kwa sasa Tanzanite ana umri wa miaka mitano na ni mwanafunzi katika moja ya shule ya awali jiji Dar.

Ukiachana na hayo, katika ukuaji, wazazi wake, wamechagua kumlea katika muonekano wa kistaa na katika makala haya, Flora anafunguka mambo mengi kuhusu mtoto wake huyo;

Over Ze Weekend: Kwa muda sasa husikiki si kwenye filamu wala muziki, umejichimbia wapi?

Flora: Nipo, hapa kati nilibanwa na malezi, si unajua tena nina mtoto mdogo, Afrika, lakini pia kwa sasa nipo chuo ninasoma kwanza.

Over Ze Weekend: Unasomea nini?

Flora: Nasomea Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (Journalism & Mass Communication).

Over Ze Weekend: Katika uigizaji ndiyo umeamua kupiga chini baada ya soko kuporomoka?

Flora: Nimeamua kuongeza tu elimu. Lakini bado ninaigiza na kuna kazi mbili zitakuja si muda mrefu. Moja, ninategemea kuifanyia uzinduzi siku si nyingi.

Mtoto Tanzanite.

MSIKIE KUHUSU H-BABA

Over Ze Weekend: Kuna kipindi umepitia changamoto za uhusiano na H-Baba, kwa sasa uhusiano wenu ukoje?

Flora: (Anacheka kisha anajibu) sipendi kuzungumzia suala hilo, lakini niseme tu ninaishi na watoto wangu wote na tuna furaha na maisha.

Over Ze Weekend: Unamaanisha H-Baba ndiyo imetoka hivyo na anahudumia familia tu?

Flora: Hatupo vizuri, kuna mambo yametokea katikati yetu, kuhusu mambo mengine tafadhali naomba niishie hapa.

Kuhusu Tanzanite je?

Over Ze Weekend: Staa mtoto anaendeleaje? (Tanzanite).

Flora: (Anatabasamu), Tanzanite yupo vizuri, anaendelea na masomo na mambo mengine.

Over Ze Weekend: Kwa nini mmechagua kumlea mtoto huyu katika maisha ya kistaa?

Flora: Kwanza Tanzanite ana kipaji. Tumegundua hilo katika siku zake za awali kabisa kwamba anapenda kuimba na kucheza. Lakini ni mchangamfu sana na ana vitu vingi ambavyo kama wazazi tuliona tukimtunza vizuri kistaa vitamsaidia huku mbeleni kwenye maisha yake hasa kwenye ulimwengu wa sanaa.

H-Baba.

Over Ze Weekend: Kama mama unapenda akikua awe nani?

Flora: Yeye mwenyewe ana haki ya kuchagua awe nani akikua. Ninachofanya nikumtunza vizuri tu na kumsaidia kuendeleza vile ninavyoona kuwa ni vipaji vyake.

Over Ze Weekend: Amekuwa akipata nafasi ya kufanya matangazo na baadhi ya makampuni lakini mengine mmekuwa mkikubali, mengine mkikataa, kwa nini?

Flora: Huyu mtoto tunamlea kistaa, kwa hiyo kiukweli ni lazima tuchague nini afanye na nini asifanye ili kumkuza vyema. Matangazo ambayo atafanya ni yale ambayo tunaona yanamuongezea mashabiki, umaarufu na kipato pia.

Over Ze Weekend: Mpaka sasa amepata na kufanya matangazo mangapi?

Flora: Amepata matangazo mengi sana, nawezi kusema ni zaidi ya mastaa wengi hapa Bongo! Hata hivyo mengine tunayakataa kwa sababu ambazo nimezisema hapo nyuma. Lakini machache aliyofanya ni pamoja na tangazo kutoka Shirika la IBM Signature kutoka Marekani, maduka ya nguo za watoto (kids fashion), tangazo la biskuti kutoka kwa Lamatta na Mtandao wa Simu za Mikononi wa Vodacom!

Over Ze Weekend: Kwa tangazo moja unachukua kiasi gani?

Flora: Bei ni maelewano, lakini sichukui chini ya milioni tatu, kwa kuzingatia vigezo vya muda wa kufanyika tangazo lenyewe, nini anatakiwa afanye, sehemu na mengine mengi.

Boniphace Ngumije.

Global TV Kenya: Moto Mkubwa Waibuka Kenya, Taharuki Tatanda

Leave A Reply