The House of Favourite Newspapers

Forbes Wamtangaza Melinda Gates Kuwa Bilionea Mpya

0

NI stori iliyowagusa wengi huku wengine wakijiuliza maswali bila kuwa na majibu baada ya ndoa ya tajiri wa Dunia Bill Gates na Belinda iliyodumu kwa miaka 27 kisha kufanikiwa kupata Watoto watatu kutangazwa kufika mwisho yaani wameachana.

 

Jana, Mei 6, 2021 kupitia mtandao wa jarida la Forbes wamemtangaza mwana Mama huyo anaefahamika kwa jina la Melinda kuwa ni Bilionea Mpya anaeshika nafasi ya 5 kwenye orodha ya Matajiri Duniani baada ya kuhamishiwa fedha kwenye akaunti yake kutoka kwenye kampuni ya Bill Gates kama mnufaika wa hisa za uwekezaji wa kampuni zake.

 

Forbes wanasema Melinda kwasasa ana Tajiri wa bilion 1.8 za kimarekani hii imekuja baada ya kuwa mnufaikaji wa hisa za uwezekaji wa kampuni ya Bill Gates.

 

Kwa mujibu wa Forbes wanasema utajiri wa Bill Gates umeshuka toka ($130.4 Bilion) hadi ($128.6 Bilion) baada ya Melinda kuhamishiwa fedha hizo lakini bado inamuweka Bill akiwa kwenye nafasi ya 4 ya orodha ya Matajiri wa Duniani huku Melinda akiwa katika nafasi ya 5 ya orodha hiyo ya Matajiri Duniani.

 

Leave A Reply