The House of Favourite Newspapers

Fraga: Huyu Bwalya Anajua Aisee

0

MKATA umeme wa Simba raia wa Brazil, Gerson Fraga Vieira amesema kuwa usajili wa kiungo mpya, Larry Bwalya kutokea Klabu ya Lusaka Dynamos ya nchini Zambia ni miongoni mwa usajili bora ambao umefanyika kutokana na uwezo mkubwa anaouonyesha kiungo huyo katika viwanja vya mazoezi vya Simba Mo Arena vilivyoko Bunju jijini Dar.

 

Simba ilianza rasmi mazoezi ya kujiandaa na msimu wa 2020/21, Jumatatu ya iliyopita hii huku wachezaji wote saba wapya wakiwa sehemu ya mazoezi hayo na kuwapagawisha mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakikusanyika kwa wingi kuwashuhudia.

 

Akizungumza na Championi, Fraga alisema: “Naupongeza uongozi kwa usajili bora ambao wameufanya kuelekea msimu ujao, baada ya kupata nafasi ya siku chache kufanya mazoezi na nyota wapya waliosajiliwa kwa upande wangu nadhani usajili huu utazidi kutufanya bora zaidi.

 

“Nimevutiwa sana na uwezo mkubwa wa kiungo wetu mpya, Larry Bwalya ambaye amekuwa kivutio kikubwa kutokana na kipaji cha soka alichonacho, naamini tutakuwa imara zaidi tutakapocheza pamoja,” alisema Fraga.

JOEL THOMAS NA LEEN ESSAU, Dar es Salaam

Leave A Reply