The House of Favourite Newspapers

Fred Lowassa Kuwapeleka Watoto Kuangalia kombe la Dunia Nchini Qatar

0
Mbunge wa Monduli, Fred Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto washiriki wa mashindano ya mchezo katika uzinduzi wa mashindano ya kombe la  (FRED LOWASSA CUP) yaliyofanyika  kata ya Meserani wilayani Monduli mkoani Arusha.

 

 

Mbunge wa  Jimbo la Monduli  Fred Lowasa ametoa ahadi ya kuwapeleka kuangalia kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022 watoto watatu wa jamii ya kifugaji kutoka wilayani humo watakaofanya  vizuri katika michuano ya mpira wa miguu ya kombe la Fred Lowassa .

 

Fred ameyasema hayo wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mashindano ya kombe la  Fred Lowassa(FRED LOWASSA CUP) yaliyofanyika  kata ya Meserani wilayani Monduli mkoani Arusha na kushirikisha timu kutoka shule 82 za msingi kutoka kata 20.

Wakiwa katika picha ya pamoja.

“Mashindano haya yatafanyika kila mwaka   na nimetoa ahadi yangu kwa kuwapeleka  kuangalia kombe la dunia mchezaji bora,mtoto mwenye nidhamu,na mfungaji bora  wote nitawapeleka kwenda kuangalia kombe la dunia na watasindikizwa na wazazi wao ,hivyo naombeni Sana mjitahidi kuonyesha vipaji vyenu mkiwa bado wadogo kwani hayo ndo maandalizi ya kuwa wachezaji maarufu Kama walivyo wengine.”alisema Fred.

 

Fred alisema kuwa, amefikia hatua ya kuzisaidia timu hizo kwa lengo la kuinua vipaji kwa watoto waliopo chini ya miaka 15 ,huku lengo likiwa ni kuhakikisha wanatoa mchezaji bora kutoka wilaya ya  Monduli ili watoto hao waweze kuwa na moyo wa kuipenda michezo wakiwa tangu wadogo.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu ,Selemani Kakoso akizungumza katika uzinduzi huo.

 

Amesema kuwa,anataka kuhakikisha michezo inapewa kipaumbele katika wilaya ya Monduli hususani kwa watoto wa shule za msingi walioko chini ya umri wa miaka 15 ili kuinua vipaji vyao kwani watoto wengi wana vipaji vikubwa ila changamoto iliyopo ni kutopata wadau wa kuviendeleza vipaji hivyo.

 

“tufike mahali sasa tuwekeze kwenye michezo kwani michezo inalipa Sana ,na napenda kuwaambia vijana hawa kuwa mpende michezo na  mjiajiri zaidi huko kwani ikitumiwa vizuri ni ajira nzuri sana  kama zilivyo ajira nyingine “alisema.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu ,Selemani Kakoso akizungumza katika uzinduzi huo amepongeza Sana jitihada zilizofanywa na Mbunge huyo ya kuinua vipaji kwani kwa kufanya hivyo wanatengeneza mazingira bora ya kukuza elimu na vijana kuweza kujiajiri kupitia michezo .

 

Aidha alimwomba Mbunge huyo kutoishia kuwekeza  kwenye mpira wa miguu pekee bali pia waifufue michezo ya riadha ambayo imefifia Sana mkoani Arusha wakati zamani ndo ilikuwa inaongoza kwa kuwa na wachezaji bora wa riadha .

 

“Unajua unapofikia hatua ya kuwekeza kwenye michezo hasa kuanzia ngazi ya chini unawasaidia  sana watoto kuweza kuinua vipaji vyao wakiwa wadogo na mimi kwa kuunga mkono juhudi za Mbunge huyu shule itakayokuwa bingwa kwenye mashindano hayo  nitaleta kompyuta tano ili kuimarisha mfumo wa Tehama mashuleni .”amesema Kakoso.

Naye Katibu wa chama cha mpira wilayani Monduli (MODFA),Abubakar Hamisi amesema kuwa,mashindano hayo ya kombe la Fred Lowassa yameshirikisha shule za msingi 82 kutoka wilaya hiyo katika kata 20 kwa ajili ya kuinua  mpira wa miguu .

 

Amesema kuwa, katika uzinduzi wa kombe hilo zimeshiriki katika Tarafa ya Kisongo zimeshiriki timu  sita za umri chini ya miaka 15 ambapo lengo kubwa ni kuhakikisha wanaijua vipaji vya watoto wakiwa tangu wadogo na kuweza kuviendeleza vipaji vyao.

 

Naye Afisa elimu msingi ,Nitabarak Mollel amemshukuru Mbunge huyo kwa namna ambavyo ameona umuhimu wa kuanzisha michezo katika wilaya hiyo ili kusaidia kuinua vipaji vya watoto hao wakiwa tangu wadogo ambapo kupitia michezo hiyo itatoa motisha wa watoto kuweza kujiandikisha shule kwani wengi wao hawajaripoti shule mpaka sasa hivi,ambapo aliomba kuanzishwa kwa mpira netball kwa wasichana pia.

 

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wabunge wengine wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu akiwemo Ally Anyigulile wa Kyela,Sophia Kagenda viti maalum Mbeya,mhe Bahati kutoka baraza la wawakilishi Zanzibar,na katibu wa kamati hiyo Hossiana ambao wote kwa pamoja walimpongeza Fred kwa kuanzisha michezo hiyo ambayo wamesema itasaidia kuibua vipaji na kuwa ajira za vijana hao baadae.

Leave A Reply