The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI MACHI 08: JPM, KAGAME Wakubaliana Haya Kuhusu Rwanda na Tanzania – VIDEO

Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Paul Kagame,amehitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Ni mapema hii leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Rais Magufuli akiambatana na baadhi ya viongozi wa serikali kumuaga mgeni wake Rais wa Rwanda ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya afrika mashariki, Paul Kagame baada ya kuhitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.

Katika Ziara hiyo viongozi hawa wamepata fursa ya kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili pamoja na kuzungumzia masuala mbalimbali yahusuyo jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hii ni ziara ya nne kwa Rais Kagame kuzuru Tanzania katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano,na ikiwa ziara ya kwanza kufika nchini akiwa mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo amesema mazungumzo yao yataimarisha umoja wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tanzania na Rwanda zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika miradi mbalimbali ambapo kwa sasa inalenga kutekeleza mradi wa reli ya kisasa SGR itakayopita Isaka hadi Kigali umbali wa zaidi ya kilomita mia tano.

Comments are closed.