The House of Favourite Newspapers

Motra The Future: Ningemsaka Harmorapa Anipe Kiki

0

MSANII wa Hip Hop anayewakilisha pande za R chuga, Motra The Future ambaye anatamba sana  na ngoma yake ya Sina Koloni aliyomshirikisha G Nako kutoka Kundi la Weusi ameibuka na kusema kuwa kama ikitokea muziki hauendi bila kiki basi yeye atachagua kiki ya kumtwanga ngumi za kutosha Harmorapa.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuulizwa kwamba kwa nini wanamuziki wengi wanapenda kutafuta kiki kila wanapotaka kutoa ngoma.

“Siamini katika kiki! Na kama ingetokea nikaambiwa kwamba siwezi kutoka bila kiki, basi ningemtafuta Harmorapa, nimtandike ngumi ili nipate kiki kwani yeye ndiye mtu wa kutafuta kiki sana mitandaoni ili afanikishe kila anachokitaka,” alisema Motra The Future ambaye kwa sasa yupo chini ya Weusi baada ya kukosa menejimenti ya kusimamia kazi zake.

Mahojiano yake mengi Zaidi unaweza kuyapata kupitia chaneli yako ya kijanja ya Global TV Online iliyopo Youtube.

Stori: Isri Mohamed

Leave A Reply