The House of Favourite Newspapers

G Nako ahamia Kwa Watoto Wa Kike

WAKATI may 28 ilikuwa ni kilele cha maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani, rapa anayefanya poa kutoka Kundi la Weusi, George Sixtus Mdemu ‘ G Nako’ ameelezea alivyofanikiwa kupitia mfuko wake wa kusaidia watoto wa kike (G Nako for the Girl Child).

 

Akizungumza katika Kipindi cha Bongo 255 kinachorushwa na +255 Global Radio, G Nako alisema kwamba, kitu alichokuwa amekianzisha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike ni endelevu hadi pale wazazi watakapopata ufahamu wa kuelewa.

 

 

“Lengo hasa mbali na kuwasaidia watoto kwanza ni wazazi waelewe nafasi yao kwa watoto wao ni ipi. Kwa sababu hili suala ukiangalia kwa undani zaidi huko vijijini utagundua wazazi wengi hawapo karibu na watoto wao wa kike.

 

“Wakati niko Arusha na projekti hii nilikuwa na shule nane, nimefanikiwa kupata taulo za kike ‘pads’ ambazo zitawatosha shule nne mpaka watakapomaliza mwaka huu kwa hiyo ni mafanikio makubwa sana,” alisema G Nako.

 

Rapa GNako (katikati) akiwa na watangazaji wa kipindi cha Bongo 255

 

G Nako pia alizungumzia muziki wa Hip Hop hasa kwa wale wanaofikiri msanii wa aina hiyo akiamua kuimba anavunja miiko ya Hip Hop.

 

“Watu wanapotosha sana. Hip Hop ni misingi ya maisha halisi, kinachotokea kama una kipaji cha kuimba, kurap au kingine kwa nini usivitumie wakati Mungu amekubariki? Huwezi kuwa unatangaza halafu una kipaji cha kurap ukafanya wakasema unavunja miiko ya Hip Hop no noo!” Alimaliza kusema G Nako.

 

Kwa mahojiano zaidi waweza kuyapata kupitia Global TV,  Ukiingia usisahau ku-subscribe na kubonyeza kengele ya pembeni yake ili usipitwe na matukio yote.

 

TAZAMA VIDEO HAPA

Comments are closed.