The House of Favourite Newspapers

MTIBWA SUGAR YAWABANA SIMBA SC

MCHEZO wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2018/2019 kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya mabingwa wa ligi hiyo, Simba Sc umekamilika xkatika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro huku timu zote zikitoshana nguvu baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.

Mgeni rasmi kwenye mchezo huo alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ambaye ndiye ameongoza Hafla ya kukabidhi Kombe la Ubingwa kwa Mabingwa wa 2018/2019 ambao ni Simba Sc.

Mashabiki wengi walijitokeza kushuhudia mchezo wa mwisho kwa timu zote mbili msimu huu kwenye ligi uwanja wa Jamhuri.

Simba wamemaliza Ligi wakiongoza kwa pointi 93 mbele ya Yanga wenye pointi 86 na nafasi ya tatu ikishikwa na Azam wny pointi 78.

Mtibwa wao wamemaliza nafasi ya tano wakiwa na jumla ya pointi 50 nyuma ya KMC wenye pointi 55.

MATOKEO

Yanga SC 0-2 Azam FC.

Coastal Union 0-0 Singida.

Ndanda 1-3 Mwadui.

JKT TZ 2-0 Stand United.

Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC.

Mbeya City 0-0 Biashara.

Mbao FC 1-1 Kagera Sugar.

Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC.

African Lyon 0-2 KMC FC

Stand United imeungana na African Lyon kushuka daraja, baada ya kufungwa 2-0 na JKT Tanzania.

Mwadui FC na Kagera Sugar zitacheza ‘Playoffs’ na Pamba FC pamoja na Geita FC kuwania nafasi ya kurejea ligi kuu.

Dakika 90 zimemalizika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Azam FC wanalipa kisasi. Yanga SC 0-2 Azam FC

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.