The House of Favourite Newspapers

GAME 1: Golden Warriors Waichapa Cleveland Cavaliers 124-114

SHUGHULI ya fainali ya Ligi ya Mpira wa Kika­pu ya Marekani (NBA) imeanza baada ya Golden State Warriors kuiliza Cleveland Cavaliers 124-114 kwenye mechi ya kwanza usiku wa kuamkia jana Iju­maa.

 

Mechi hiyo ili­kuwa kali huku kipindi cha kwanza kikisisimua zaidi, ambapo timu zote mbili zilikuwa zi­najaribu kufunga pointi kwa mitupo ya mbali.

Kipindi cha pili kilikuwa kikali zaidi, ambapo Golden S t a t e w a l i ­s h a m ­b u l i a v i k a l i h u k u C a v a ­l i e r s wakilaz­imika ku­zuia pre­sha hiyo kali.

 

Mc h ­ezo huo u l i i n g i a dosari ka­tika dakika za mwisho baada ya staa wa Cava­liers Tristan T h omp s o m kutolewa na mwamuzi, am­bapo wachezaji wa pande zote walizongana kutaka kupigana.

 

Pamoja na LeBron James kuifungia Cavavlier pointi 51 na kutoa asisti nane bado hazikusaidia timu hiyo kuibuka na ushindi.

 

Staa wa Warriors, Steph Curry alifungia timu yake pointi 29 wakati Draymond Green aliongeza pointi 13 na ku­toa asisti tisa.

 

Timu hizo zitavaana kwenye mechi ya tatu ya fainali ya ligi NBA kes­hokutwa Jumatatu.

Warriors itaikaribisha Cavaliers kwenye uwanja wao wa Oracle Arena ambapo itawania kushin­da tena ili kuongeza ma­tumaini yao ya kutetea taji lao.

Comments are closed.