The House of Favourite Newspapers

Gari La Abiria Lagongwa, Watu 9 Wafariki, 23 Wajeruhiwa Mbeya

0

Ajali imetokea katika Mteremko wa Iwambi, Mbeya Vijijini baada ya Lori aina ya Howo la #Zambia likiendeshwa na Mohamed Abilah (47) kuligonga kwa nyuma Basi dogo aina ya Mitsubish Rosa likiendeshwa na Elly Elia Mwakalindile (41)

Chanzo cha ajali hii ni Dereva wa Lori kushindwa kulimudu gari kwenye mteremko mkali na kwenda kuigonga kwa nyuma Basi hilo. Dereva wa Lori amekamatwa na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika

Waliopoteza maisha ni Wanaume 5 na Wanawake 4, waliojeruhiwa ni Wanaume 13 na Wanawake 10. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema majeruhi wanatibiwa Hospitali Teule ya Ifisi ya Mbalizi na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, miili imehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi

Leave A Reply