The House of Favourite Newspapers

Gari la Mbunge Lachomwa Moto Usiku

0

 

Gari la Mbunge wa Mbozi, mkoani Songwe, George Mwenisongole aina ya Brevis lenye namba za usajiri T231 DDZ  limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Septemba 29, 2021, nyumbani kwa mbunge huyo, Ichenjezya Mjini Vwawa mkoani Songwe.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni majirani wa eneo hilo wanasema mnamo majira ya saa 9 usiku walisikia mlipuko na baada ya kutoka nje walikuta gari ikiwaka moto.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omari Mgumba amesema chanzo cha tukio bado hakijajulikana na wameviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kisha wahusika wakipatikana watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, tukio hilo lina sura ya vita ya kisiasa kwani kwa takribani miezi miwili sasa amekuwa akilala nje na nyumbani hapo kwa kuhofia usalama wake. Amesema majirani walisikia mbwa walikuwa wakibweka kwa muda kama nusu saa na baada ya hapo ukimya ulitawala na ndipo walipotoka nje wakakuta gari linawaka moto.

Mwenisongole amesema kwa miezi miwili sasa amekuwa akilala maeneo tofautitofauti kwani kuna watu anahisi wamekua wakimfuatilia maisha yake hivyo wakati tukio linatokea hakuwepo nyumbani kwake.

Leave A Reply