The House of Favourite Newspapers

Safari ya Maisha ya Fredy Vunjabei na Frank Knows

0

KUPITIA ukurasa wa Instagram tajiri kijana anayemiliki maduka ya nguo Dar es Salaam na mikoa yote, ameshare story yake na rafiki yake kipenzi Frank Knows Wakali kutoka Too much Money.

 

“Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa na duka moja dogo sana Kariakoo (Goli), baada ya kujikusanya tulikubaliana na rafiki yangu Frank Knows twende kujaribu kununua mzigo China, tulisubiri kipindi cha tiketi za offer na tukapata Ethiopian Airways.

 

“Tulifanikiwa kufanya utafiti wa maana sana China na tukajilaumu tulikuwa wapi siku zote, Ndoto zangu nlianza kuziona zikikamilika licha ya kuwa China ilitakiwa uwe na hela nyingi na wote tulisafiri na pesa kidogo sana hazikutosha kununua mzigo.

 

“Nilitafakari nifanye nini? hesabu zetu zilionesha kununua mzigo mdogo China ni kazi bure na hela itapotea, mwisho wa siku niliamka asubuhi nkamuita Frank nikamwambia “Nimeamua kukupa hela yangu yote ukifanikiwa utanishika mkono ukifeli tutakuwa tumejifunza kitu” alinishangaa sana.

 

“Alipojumlisha na yake jumla ikawa million kumi na mbili (12mil), Nlifanya hivyo kwa sababu zifuatazo. Moja, Nilijua lazima mmoja wetu akubali kuwa na subira na mwingine atangulie (urafiki wetu hatukuwahi kuweka wivu na ubinafsi mbele).

 

Pili, Frank alikuwa na wateja wengi kuliko mm hivyo angezungusha hela haraka zaidi. (Ni vema kukubali ukweli). Nilimuacha Frank akazungusha hela kwa muda kama wa miezi 6 na alikuwa akisafiri mara kwa mara.

 

“Nilifurahi kumuona akifanikiwa na nilimsaidia sana kutafuta wateja na kumshauri, baada ya hapo alikuja akanipa 20,000,000/= (Cash) na tukaondoka wote tukaenda China kufunga mzigo. Nilifunga mzigo mzuri sana sababu Frank alipata experience kubwa na alikuwa ananionesha masoko mazuri bila kuona wivu,” amesema Fredy.

Leave A Reply