The House of Favourite Newspapers

Gavana Bill Richardson Afariki Dunia, Aliwahi Kuwa Balozi wa Marekani

0

Kabla ya kuchaguliwa kwake mwaka 2002 kama Gavana, Richardson alikuwa balozi wa Umoja wa Mataifa na waziri wa nishati chini ya Rais Bill Clinton na alihudumu kwa miaka 14 kama mbunge anayewakilisha New Mexico

Bill Richardson, gavana wa mihula miwili mdemokrat wa New Mexico aliyewahi kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ambaye alijitolea maisha yake baada ya kustaafu siasa kufanya kazi kutafuta suluhu ya Wamarekani waliokamatwa nje ya nchi amefariki dunia .

Alikuwa na umri wa miaka 75. Kituo cha Richardson for Global Engagement, alichoanzisha na kukiongoza kilisema katika taarifa yake Jumamosi kwamba alifariki dunia akiwa usingizini nyumbani kwake Chatham, Massachusetts.

Kabla ya kuchaguliwa kwake mwaka 2002 kama Gavana, Richardson alikuwa balozi wa Umoja wa Mataifa na waziri wa nishati chini ya Rais Bill Clinton na alihudumu kwa miaka 14 kama mbunge anayewakilisha New Mexico. Richardson pia alisafiri kote ulimwenguni kama msuluhishi asiye rasmi wa kidiplomasia, akitafuta suluhu ya kuachiliwa kwa mateka na wanajeshi wa Marekani kuanzia Korea Kaskazini, Iraqi, Cuba hadi Sudan.

SIMBA vs AHLY: AHMED ALLY BAADA ya KUPANGIWA AHLY AFL CHEKI TAMBO ZAKE…

Leave A Reply