The House of Favourite Newspapers

Gavana BoT: Huwezi Kutumia Fedha za Ndani Kwenye Miradi

0

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga amesema Mikopo haikopwi kwa ajili ya kula bali kufanya Miradi ambayo itaendelea kuzalisha na kuleta uhimilivu mzuri wa deni

 

Profesa Luoga amesema hayo leo Jumatano, Desemba 29, 2021 wakati akihojiwa na moja ya chombo cha habari nchini ambapo ameeleza kuwa;

 

“Nchi haiwezi ikaweka rehani watu au rasilimali zake na inazitumia ili Serikali iendelee kupata kipato. Unapokopa mkopo hukopi kwa ajili ya kula unakopa kwa ajili ya kufanya project ambazo zitaendelea kuzalisha na kwasababu unaendelea kuzalisha uhimilivu wako wa deni unaendelea kuwa mzuri sio kwamba deni linapanda.

 

“Katika kamati mnaangalia madeni yenu yasiuze nchi ndio maana nchi haiwezi ikaweka rehani watu au rasilimali zake na itahakikisha inazitumia ili kuhakikisha Serikali inaendelea kupata kipato.

 

“Ukitumia pesa za ndani peke yake utapandisha kodi, utawafanya wananchi wachangie kwa njia nyingine ambayo ni gharama na itachukua muda mrefu. Badala ya kutengeneza mradi kwa miaka 3/4 utautekeleza kwa miaka 20 kwa sababu unategemea uchukue pesa za ndani, kwa hiyo hata huo mradi hautakuwa na manufaa kwako immediately,” amesema Profesa Luoga.

Leave A Reply