The House of Favourite Newspapers

Gazeti la Betika Laendelea Kusambaa Mitaani

WADAU mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu na kubashiri matokeo nchini yametolea ufafanuzi juu ya Gazeti la Betika ambalo ni bora katika takwimu za kubashiri matokeo ya michezo tofauti.

 

Wakizungumzia juu ya gazeti hilo, baadhi ya wasimamizi wa Kampuni ya SupaBeti wame­pongeza kazi nzuri inayofanywa na Betika kwa kuwa na takwimu zilizoshiba kwa ajili ya kumshibi­sha mteja wa kubashiri mechi.

 

Mmoja wa watoa huduma wa SupaBeti ambao tawi mlao lipo mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam, ambaye hakuwa tayari kutaja jina kwa kuwa siyo msemaji wa kampuni hiyo alisema Gazeti la Betika ni zuri na kushauri liongeze baadhi ya takwimu za mechi za soka.

Upande wa wawakilishi wa Kampuni ya Premierbet tawi la Makumbusho jijini Dar es Salaam, walishauri gazeti hilo kuanza kutoka zaidi ya mara moja kwa wiki, kwa sasa linatoka mara moja kwa wiki ambayo ni Jumatano.

Walipendekeza siku ya Juma­mosi kwa kuwa ni siku ambayo huwa ina mechi nyingi zaidi na watu wanapenda kubeti siku hiyo.

 

Kuhusu changamoto za kazi zao, alisema ni kwenye kutam­bua umri wa wale ambao hawa­husiki: “Ukibainika unawahudu­mia hadi wale waliochini ya umri wa miaka 18 serikali inakuchuku­lia hatua kali na hapa wanal­enga zaidi wanafunzi ambao hawaruhusiwi kabisa kushiriki michezo hii.

“Mara nyingi tunawatambua wakiwa na sare za shule tu ila wakibadilisha wengine inakuwa ngumu kuwatambua kwa sababu wanamiili mikubwa labda wale wenye miili midogo ndiyo in­akuwa rahisi kuwatambuwa.”

 

Akizungumza baada ya maoni hayo, Ofisa Masoko wa Gazeti la Betika, Kezilahabi Peresi alisema watayafanyia kazi maoni hayo na kusisitiza kuwa ndani ya Be­tika wasomaji watapata makala kali za burudani na michezo bila kusahau hadithi ya kusisimua.

 

“Tunaendelea kukaribisha maoni na wale wote wanaohitaji kutangaza nazi tunapatikana kupitia namba 0755-826488, 0712-595636 na 0659-472001 au kupitia barua pepe beti­[email protected],” alisema.

 

 

Comments are closed.