The House of Favourite Newspapers

Genevieve, D’Banj wadaiwa kurudiana

0

genevieve-and-dbanjMwigizaji maarufu wa kike wa Nigeria, Genevieve Nnaji akiwa na D’Banj.

KUNA uvumi kwamba uhusiano baina ya mwigizaji maarufu wa kike wa Nigeria, Genevieve Nnaji, na mwimbaji D’Banj wa Nigeria, wamerudisha uhusiano wao wa kimapenzi ulioanza mwaka 2010 lakini baadaye ukavunjika na kila mtu kuchukua hamsini zake.

Blogu ya JJC Skillz imedai kwamba uhusiano huo ulivunjika baada D’Banj kuonekana alikuwa hana mpango wa kumuoa Genevieve, licha ya kimwana huyo kusema alikuwa anampenda mwanamuziki huyo maarufu.

Tangu kuachana na Genevieve, D’Banj amekuwa akihusishwa na mrembo mmoja aitwaye Adama Indimi, ambaye ni binti wa mfanyabiashara mmoja bilionea aitwaye Alhaji Mohammed Indimi. Pia amehusishwa na mrembo mmoja wa Afrika Kusini ambaye jina lake halikutajwa.

Hata hivyo, D’Banj alisema wakati fulani uliopita kwamba angemwoa Genevieve, lakini mwigizaji huyo alisema katika mahojiana mwaka jana kwamba asingeweza kuolewa na mwanamuziki huyo.

Genevieve aliwahi kusema: “Kwanza kabisa lazima nikubaliane na nafsi yangu kwamba ni kweli nataka kuolewa. Kweli tutaoana, sijui. Nafikiri maisha yangu tayari yameparaganyika. Hivyo nasema jibu ni hapana.”

Uvumi kuhusu wawili hao ulienea kwamba, uhusiano wao ulikuwa umeharibika vibaya kiasi kwamba walikuwa wanakwepana katika matukio ya wazi, lakini mwaka 2015, walianza kuwa pamoja katika tukio moja na pakavuma kwamba tayari walikuwa wamerudisha uhusiano wao wa kimapenzi.

Hivi sasa uvumi huo umepamba moto kwani Genevieve amekuwa akionyesha upendo wake wa Kokomaster huyo. Hata hivyo, mashabiki wa wapenzi hao bado hawana uhakika wa wazi wa kile kinachotokea kati yao.

Leave A Reply