The House of Favourite Newspapers

Breaking: Ghorofa Lateketea kwa Moto Kariakoo – Video

JENGO moja la ghorofa lililopo Kariakoo, Mtaa wa Livingstone na Mkunguni linawaka moto mchana huu wa Jumamosi, Novemba 2, 2019 huku chanzo kikiwa hakijajulikana bado.

Tayari Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji kimeshawasili na juhudi za kuuzima moto zinaendelea

 

Imewachukua saa mbili kikosi cha zima moto kufika kuzima. Moto umeanza kuwaka gorofa ya nne muda wa saa saba.

Kikosi cha zima moto na uokoaji wanaendelea kuuzima moto katika mazingira magumu.

Hadi sasa maji yamewaishia huku moto ukiendelea kuwaka gorofa ya nne inayodaiwa ni Godauni. Chanzo cha moto hakijajulikana bado.

 

 

Comments are closed.