The House of Favourite Newspapers

GIGY ABWATUKA KUNASA KIBENDI

Gift Stanford ‘Gigy Money’

MSANII wa filamu Bongo Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kutokana na uvumi uliopo kwamba amenasa kibendi na kusema watu waache kumjadili juu ya ishu hiyo sababu mimba si kitu cha matangazo na wala haina kificho.

 

Akipiga stori na Star Mix, mwanadada huyo ambaye kitumbo chake kinaonekana kimeshiba tofauti na kawaida yake huku mwili wake ukianza kunawiri wakati alikuwa amepungua na kuzua mjadala, alisema suala hilo halimhusu mtu yeyote sababu iwe kweli au si kweli hakuna atakayemsaidia kulea.

 

“Kama nina mimba au sina haimhusu mtu, sababu mimba si kitu cha matangazo, kama ni kweli ninayo mtajua tu maana hainaga kificho, kuhusu mwili wangu kuanza kuongezeka kipindi cha nyuma nilikuwa na ‘stress’ sasa hivi niko sawa ndiyo maana nimeanza kunenepa,”alisema.

Stori: Mayasa Mariwata

LIVE: BIRTHDAY YA WOLPER! Mtazame Akikata Nyonga za Kufa Mtu!

 

LIVE: Birthday ya WOLPER! Alivyoingia Ukumbini kwa Mbwembwe!