visa

GIGY AWAKA KISA MPENZI WAKE

MSANII wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amewaka vibaya kwamba watu waache kufuatilia maisha yake na badala yake wafanye mambo yatakayowaingizia faida na siyo kumfuatilia yeye kila siku. Gigy ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kuhusu ishu yake ya kufuta picha zote za mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Hunchy katika ukurasa wake wa Instagram na kudaiwa kurudiana na zilipendwa wake Mourad alpha ‘Mo J’.

Mrembo huyo hodari kwa maneno ya shombo alisema, ameamua kufuta picha za mpenzi wake huyo kwenye akaunti yake kwa sababu zake binafsi, hivyo anashangazwa

na maneno ya watu wanaposema kuwa wameachana ndio sababu kaamua kuzifuta. “Hivi kwa nini watu huwa wanashindwa kuniacha na maisha yangu jamani, kila siku wanazua mambo mapya kwangu, sasa kwani nikifuta picha za huyo mwanaume wangu kwenye akaunti yangu kuna shida gani, kwa sababu hata nilipoanza kuziposti hawakunishauri, niliamua mwenyewe.

“Naomba kama kweli ni mashabiki wangu basi waendelee kunisapoti kwenye muziki wangu na sio kufuatilia mambo yangu binafsi, sipendi jamani na kuhusu kurudiana na Mo J sio kweli kwa sababu kila mtu sasa hivi ana maisha yake,” alisema Gigy.
Toa comment