The House of Favourite Newspapers

Gkanji: Simba Tutafika Nusu Fainali CAF

0

KIUNGO mpya wa Simba, Doxa Gkanji, amesema malengo yake ndani ya timu hiyo ni kuisaidia kufi ka mbali katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwezekana kuivuka rekodi ya msimu wa 2018/2019 ambao Simba ilifi ka robo fainali.

 

Msimu huu, Simba imetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mi-chuano inay-osimamiwa na Shirik-isho la Soka Afrika (CAF).

 

Imepangwa Kundi A na timu za Al Ahly, AS Vita na El Marreikh.Akizungumza na Spoti Xtra, kiungo huyo alisema anafahamu kuwa malengo ya timu hiyo ni kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa, hivyo atahakikisha anaisaidia kufi ka mbali zaidi ya hapo awali.

 

“Simba naifahamu, nakumbuka kuna msimu ilifi ka hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo nikiwa kama mchezaji mpya wa Simba nitafanya kila liwezekanalo nikishirikiana na wenzangu kuwa sehemu ya mafanikio mapya ikiwezekana kuivunja rekodi yao ya robo fainali na kufi ka nusu fainali,” alisema

 

kiungo huyo.Gkanji kwa sasa yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kinachoshiriki michuano ya CHAN inayoendelea nchini Cameroon.

Leave A Reply