The House of Favourite Newspapers

Global FC Kuifundisha Mpira Sinza Boys

MATAJIRI wa Sinza, Timu ya Global FC leo Ijumaa itacheza mechi ya kirafiki na wapinzani wake wa muda mrefu, Sinza Boys kwenye Uwanja wa CCM Sinza Lion jijini Dar.

 

Global FC chini ya udhamini wa Ashish Cinematographer imekuwa na rekodi nzuri kwenye uwanja huo ambapo mara ya mwisho kuutumia uwanja huo wa Sinza Lion, waliibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Sinza Veteran.

 

Mshambuliaji wa Global FC, Michae Momburi ameliambia Championi Ijumaa kuwa timu yao imejipanga kuendelea kutoa kipigo na burudani za soka la kuvutia, hivyo wapinzani wajiandae kwani atashusha muziki wote ili kulinda heshima yao.

“Tupo vizuri kuhakikisha tunapata ushindi wetu na kama unavyofahamu tukiwa kwenye Uwanja wa CCM Lion huwa hatufungwi hovyo, hivyo wapinzani wajiandae sawasawa,” alisema mshambuliaji huyo ambaye aliwahi mfungaji bora huko Moshi.

 

Baadhi ya silaha ambazo Global FC inatarajiwa kuzishusha leo ni pamoja na beki matata, Omary Mdose, straika Saleh Jembe, kiungo Wilbert Molandi na beki ‘katili’ Sweetbert Lukonge.

Comments are closed.