The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI: CHADEMA YALIA KUTEKWA MGOMBEA WAO WA UDIWANI

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelaani kitendo cha mwanachama wake, Athanas Makoti, ambaye ni mgombea udiwani katika kata ya Buhangaza wilayani Muleba kutekwa na watu wasiojulikana na kumtaka kujitoa katika kinyang’anyiro cha udiwani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dtk. Vincent Mashinji, amesema jeshi la polisi linatakiwa kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini waliomteka mgombea huyo wa udiwani.

Amesema kuwa Makoti alitekwa Februari 2 mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha na kupatikana Februari 5 akiwa ametelekezwa eneo la Hospitali ya Kagando iliyoko Muleba ambako mpaka sasa ndipo amelazwa.

 

Amesema kuwa watekaji walimteremsha katika bodaboda aliyokuwa amepanda wakati akitokea kwenye mchakato wa kampeni za udiwani ambapo watekaji hao walikuwa ndani ya gari aina ya Toyota RAV 4.

Ameongeza kuwa Makoti alitakiwa kukukubali kupokea pesa ambazo walikuwa nazo ili aweze kujitoa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani lakini baada ya kukataa ndipo alianza kusulubiwa hadi hapo walipotimiza azima yao.

Comments are closed.