The House of Favourite Newspapers

WASHINDI 2,000 WAIBUKA KIDEDEA SMATIKA YA AIRTEL

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando,(katikati) akiwapigia simu washindi wa  Yatosha SMATIKA Internet  baada ya kuchezeshwa droo kwa kuwapatia bando la Intanenti yenye GB 1 kwa kila mmoja.

SIKU chache baada ya  kuzindua promosheni ya Yatosha Internet kwa  wateja wanaonunua vifurushi vya bando la Yatosha SMATIKA Internet, watumiaji wa mtandandao huo wa  Februari 5 na 6 mwaka huu, kampuni ya simu za mkononi, Airtel Tanzania,  imewazawadia wateja  2,000  baada ya kuchezeshwa droo kwa kuwapatia bando la Intanenti yenye GB 1 kwa kila mmoja.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando, amesema kampuni hiyo imeamua kutoa zawadi kwa wateja wake wanaotumia bando la SMATIKA Internet kutokana na kuendelea kutumia huduma zao.

 

Mmbando amesema promosheni hiyo ya Yatosha Internet  itakuwa ni ya muda wa siku 30  ambapo kutakuwa na droo tatu za kila wiki siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

 

“Kwa ndroo ya kila siku wateja 1,000 watajishindia bando la Internet yenye 1 GB kwa kila mmoja, wakati droo kubwa itakuwa na washindi 10, huku watano wakijishindia simu za Smartphone na wengine watano  kujinyakulia modem,”amesema Mmbando.

 

Aidha amewataka wateja wao kutokuwa na hofu katika mchakato mzima wa uendeshaji wa promosheni hiyo kwani ni ya wazi na inasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha  nchini.

 

 

 

Comments are closed.