The House of Favourite Newspapers

Global Habari Dec 08 – Mwili Wa Jaji Nsekela Waagwa Dodoma

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameongoza wakazi wa Dodoma kuuaga mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela aliyefariki Dunia Decemba 6 Mwaka huu. Ibada ya kuuaga mwili wa Jaji Nsekela imefanyika leo Dec 8, 2020 katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma huku ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.

 

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika ibada ya Hiyo, ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, pamoja na viongozi mbalimbali wa Dini.

 

Marehemu Jaji Mstaafu Nsekela alizaliwa Oktoba 21 mwaka 1944, nakufariki Dec 6 mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi, mwili wake unatarajiwa kuzikwa kule jijini Mbeya Siku ya Alhamisi. Jaji Mstaafu Harold Nsekela ameacha mke, watoto na wajukuu. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT AMAZON: https://www.amazon.com/shop/globaltvo…

Leave A Reply