The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 05: Miaka 42 ya CCM, JPM, Mkewe Watinga Channel 10 – VIDEO

Rais John Pombe Magufuli amevitaka vyombo vya habari kuwa huru kuzungumzia jambo lolote ikiwa ni pamoja na kufichua mambo yaliyojificha bila kuwa na woga wowote.

Rais Magufuli amesema hayo leo February 5 alipofanya ziara katika vyombo vya habari vya African Media Group ikiwemo Kituo cha redio cha Magic FM pamoja na kituo cha Runinga cha Channel Ten ikiwa leo ni maadhimisho ya maika 42 ya chama cha mapinduzi CCM Tangu kilipoanzishwa mwaka 1977.

Rais Magufuli amefanya ziara hiyo akiambatana na Mkewe mama Janeth Magufuli kujionea utendaji wa kazi unavyoendelea kwenye vituo hivyo.

Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kusikiliza taarifa ya utendaji na kero mbalimbali wanazokabiliana nazo, Magufuli amewataka kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha kampuni hiyo inapiga hatua kiushindani huku akiiahidi kampuni hiyo kuipatia jengo zuri la kufanyia kazi.

African Media Group inayojumuisha Magic FM pamoja na Channel Ten kwa sasa ni Mali ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

Comments are closed.