The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI: PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA SABABU HIZI HAPA

GLOBAL HABARI: PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA SABABU HIZI HAPA Serikali imesema kuwa inatarajia kufikia lengo la ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7.0 kwa mwaka 2017/2018 kutokana na mwenendo wa ukuaji wa pato la taifa ambapo hadi sasa ukuaji wa pato hilo unaonesha kuwa limeongezeka kwa asilimia 6.8.

 

Takwimu hizo zimetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akisoma hotuba ya kuahirisha Bunge , ambapo amezitaja sekta zilizochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa pato hilo kuwa ni pamoja na Habari na Mawasiliano, Uchimbaji madini, Biashara, Uzalishaji viwandani na Ujenzi.

 

Waziri Mkuu amezungumzia pia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kipindi cha nusu mwaka cha bajeti ya serikali. Hoja hiyo ya kuahirisha Bunge imeungwa mkono na hivyo Naibu spika ameliahirisha bunge hilo hadi April 3 mwaka huu ambapo mambo mbalimbali yanatarajiwa kujadiliwa ikiwa ni pamoja na bajeti ya serikali.

Comments are closed.