The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI: SUMAYE AICHARUKIA TUME YA UCAGUZI

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa CHADWMA Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia sheria na kutoa uwanja sawa wa ushindani katika uchaguzi mdogo wa wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Feb. 17 mwaka huu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Sumaye amesema, wasimamizi wa uchaguzi huo mdogo wamekuwa wakifanya maamuzi kinyume na matakwa ya sharia na kanuni za uchaguzi na yamekuwa yakiwakandamiza Zaidi wao.

 

Kwa upande wake mkurugenzi wa oparesheni wa CHADEMA, Benson Kigaia amesema, tume imekuwa ikivunja kanuni za uchaguzi kwa kukikandamiza chama hicho.

 

Kampeni za uchaguzi kwa majimbo ya Kinondoni na Siha zinaonekana kuwa na mvutano mkubwa huku vyama vya CCM na CHADEMA vikionekana kuchuana kwa ukaribu Zaidi.

Comments are closed.