The House of Favourite Newspapers

Global Publishers App Yamwaga Zawadi Valentine’s Day

Washiriki waki-install Global Publishers App kwenye simu zao.

 

APPLICATION ya Global Publishers inayopatika kwenye smartphones zote za Android na iOS imezidi kutikisa mitandaoni huku ikiteka maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali za duniani kujiunga na App hiyo ya kijanja ambayo inaongoza nchini kwa habari na matukio ya papo kwa hapo.

Katika shngwe za usiku wa wapendanao, Valentine’s Special zilizofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live usiku wa kuamkia leo Feb. 15, 2018 ambapo palikuwa na shoo ya kibabe iliyogongwa na Msaga Sumu, Jahazi Modern Taarab, Classic Dalada na wengine kibao, huku mashabiki na wadau waliokuwepo ukumbini huku wakijinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo tisheti na  baada ya ku-install Global Publishers App.

Mshindi akitangazwa papo hapo.

 

Baada ya kupakua na ku-install Global Publishers App, mashabiki walijiunga na Global TV Online kwa ku-subscribe ambapo washindi wote walizawadiwa T-Shirt mpya za Global Publishers App kama wanavyoonekana pichani.

 

Muonekano wa Global Publishers App kwenye simu.

Ndani ya Global Publishers App kuna habari za matukio mbalimbali ya kijamii ndani na nje ya nchi, matukio ya papo kwa hapo, Global TV Online, simulizi, hadithi na vitabu vya mtunzi mahiri, Eric Shigongo, magazeti yote ya Global Publishers, video za nyimbo zote mpya za Bongo Fleva na za mamtoni.

Mshindi akielezea furaha yake baada ya kuibuka kidedea.

 

Zoezi likiendelea.

 

Install

Android: ==>

iOS: ==>

Comments are closed.