The House of Favourite Newspapers

GLOBAL PUBLISHERS APP YAMWAGA ZAWADI ZA BEATS BY DRE, PASAKA

APPLICATION ya Global Publishers inayopatika kwenye smartphones zote za Android na iOS imezidi kutikisa mitandaoni huku ikiteka maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali za duniani kujiunga na App hiyo ya kijanja ambayo inaongoza nchini kwa habari na matukio ya papo kwa hapo.

Katika USIKU WA SHOO YA MWISHO WA UBISHI, iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live usiku wa kuamkia leo palikuwa na shoo ya kibabe iliyogongwa Jahazi Modern Taarab, Yah TMK Taarab, Sholo Mwamba na Man Fongo.

 

Mashabiki na wadau waliokuwepo ukumbini hapo na ambao tayari wameshapakua application ya Global Publishers wakijinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo tisheti na zawadi kubwa kabisa ya Headphones za Kijanja za Beats by Dre Orijino kutoka Marekani zilitolewa na Global Publishers App.

Baada ya kupakua na ku-install Global Publishers App, mashabiki walijiunga na Global TV Online kwa ku-subscribe ambapo washindi wote walizawadiwa T-Shirt mpya za Global Publishers App kama wanavyoonekana pichani.

Ndani ya Global Publishers App kuna habari za matukio mbalimbali ya kijamii ndani na nje ya nchi, matukio ya papo kwa hapo, Global TV Online, simulizi, hadithi na vitabu vya mtunzi mahiri, Eric Shigongo, magazeti yote ya Global Publishers, video za nyimbo zote mpya za Bongo Fleva na za mamtoni.

Shuhudia picha hizo.

Comments are closed.