The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba: Washindi wa Pikipiki, Televisheni, Simu Wakabidhiwa Zawadi Zao (Live Video)

WATU watano walioshinda katika droo ndogo ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba iliyofanyika Februari 8, leo wamekabidhiwa zawadi zao katika ofisi za Global Publishers (wachapishaji wa Magazeti ya Amani, Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Risasi Mchanganyiko na Uwazi), zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo tukio hilo limerushwa moja kwa moja kupitia YouTube Channel ya Global TV Online.

Mwakilishi wa TSN akimkabidhi mshindi wa Dinner Set, Gasper Peter (kushoto).

Washindi hao ni Andrew Mtunguja wa Muheza Tanga aliyejishindia pikipiki, Ambrosi Mgonja wa Mang’ula mkoani Morogoro aliyejishindia televisheni, Evans Stanley wa Kunduchi na Said Mohamed wa Kimara Dar ambao wote wamejishindia simu za kisasa (smartphones) na Gasto Peter wa Kimara pia aliyejishindia Dinner Set (vyombo vya jikoni).

Mwakilishi wa British School akikabidhi zawadi ya smartphone kwa mshindi, Said Mohammed (kushoto).

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Amran Kaima akikabidhi zawadi ya smartphone kwa mshindi, Evans Stanley (kulia).

Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula akikabidhi zawadi ya TV –  flat screen kwa mshindi, Kisoda Ambrose (kulia).

Mr. Shinda Nyumba, akimkabidhi funguo za pikipiki mshindi, Andrew Mtunguja (kulia).

Mtunguja akikabidhiwa kadi ya pikipiki na Mr. Shinda Nyumba.

Mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao, baadhi wa washindi wa Droo ya Kwanza ya Shindano la Pili la Shinda Nyumba walipata wasaa wa kuelezea furaha zao kutokana ushindi walioupata.

Kwa upande wake mshindi namba moja wa droo hiyo aliyejinyakulia pikipiki mpya yenye vibali vyote, Andrew Mtunguja alisema haya.

“Nimefurahi sana kushinda pikipiki, nilishawahi kucheza mara nyingi sana mashindano kama haya lakini sikubahatika kushinda, mpaka siku nilipopigiwa simu kuambiwa kuwa nimeshinda pikipiki, nilimwambia mke wangu lakini hakuamini, akaniambia nimepigiwa simu na matapeli.

“Lakini leo  nimeamini kuwa ni kweli zawadi zinatolewa wala hakuna cha utapeli, mimi nimetoka Tanga na leo naondoka na pikipiki yangu mpya, hivyo niwasihi Watanzania wote waamini hiki kitu ni cha kweli kabisa na siyo mambo ya kupeana zawadi kwa kufahamiana kama tunavyoamini mitaani.”Alisema Mtunguja.

Naye Meneja Masoko wa Global Publishers, Davis Mwaipaja akizungumza wakati wa hafla hiyo.

 

Naye Meneja Masoko wa Global Publishers, Davis Mwaipaja amewasihi Watanzania wote kushiriki shindano hili kwa kununua Magazeti ya Global Publishers na kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili wa kila Gazeti lililotajwa hapo juu, kuizaja  na kuituma kwenye Ofisi za Global kwa kufuata maelekezo.

“Watu wameamini kuwa Global Publishers tunachokisema, tunamaanisha, magazeti yetu sita yanakupa nafasi kubwa ya kuwa mshindi na yote yana nafasi sawa ya kukufanya uwe mshindi.

“Leo tumetoa pikipiki ya kwanza kwa mshindi (Mtunguja) ambaye ataondoka nayo kwenda Tanga, bado kuna pikipiki nyingi zinakuja kwenye droo zijazo kwa ajili ya Watanzania, na kikubwa zaidi ni  mshindi wa droo kubwa ya shindano hili ambaye atajinyakulia nyumba mpya pamoja na samani zake ndani,

“Hivyo niwaombe Watanzania wote washiriki kwa moyo mmoja shindano hili kwani kwa shilingi 500 tu utashinda pikipiki mpya, vyombo vya ndani, simu na nyumba mpya na fenicha zake, kadri unavyojaza na kutuma kuponi nyingi zaidi ndivyo unajipa nafasi ya kujishindia zaidi.” Alisema Mwaipaja.

Mwakilishi wa Bristish School akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mshindi wa SmartPhone, Evans Stanley akielezea furaha ya ushindi wake kwenye droo ya kwanza ya Shinda Nyumba.

Gasper Peter mshindi wa dinner set akielezea furaha yake.

Mr. Shinda Nyumba akikabidhi funguo za pikipiki kwa mshindi, Andrew Mtunguja.

Mshindi akikabidhiwa funguo na kadi ya pikipiki.

Andrew Mtunguja akiwa amepanda kwenye pikipiki aliyoshinda.

Washindi wote kwenye picha ya pamoja na Mr. Shinda Nyumba.

Picha zote na Sweetebert Lukonge | Global Publishers.

Comments are closed.