The House of Favourite Newspapers

Global TV Yatinga Sauzi, Yashuhudia Messi na Suarez Wakiiangamiza Mamelodi- Video

TELEVISHENI namba moja ya mtandaoni nchini, Global TV Online imetinga nchini Afrika Kusini kushuhudia mchezo wa Kombe la Mandela uliopigwa jana kati ya Mabingwa wa Laliga ya Hispania, Barcelona na Mabingwa wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns katika uwanja wa Soccer City, karibu na Jiji la Johannesburg.

Katika mchezo huo, Barca waliibuka na ushindi wa bao 3-1 huku wafungaji wakiwa ni Ousmane Dembele, Luis Suarez na Andre Gomes na bao la kufutia machozi la Mamelodi likifungwa na Sibusiso Vilakazi.

Lionel Messi yeye aliingia akitokea benchi, alishangiliwa na mashabiki wa Barca nchini humo na hata wale wa Mamelodi kulingana na umaarufu wake.

Mechi hiyo ilikuwa ni sehemu ya nchi ya Afrika Kusini kusherehekea miaka 100 tangu kuzaliwa kwa muasisi wa Taifa hilo, Marehemu Mzee Nelson Madiba Mandela aliyweaga dunia Desemba 2013 akiwa na miaka 95.

 

Tazama Global TV ilivyoshuhudia mchezo huo.

Comments are closed.