The House of Favourite Newspapers

Global Yamkabidhi Kamanda Mambosasa Tuzo ya Heshima

KAMPUNI ya Global Publishers, juzi Jumatano ilimkabidhi Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Tuzo ya Heshima kutokana na kutambua mchango wake wa kuliweka Jiji la Dar es Salaam katika hali ya utulivu.

 

Kamanda Mambosasa alikabidhiwa tuzo hiyo alipotembelea Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Wakati anawasili ofisini hapo, alipokewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo na kupita kwenye zuria jekundu. A

 

kiwa ndani ya kampuni hiyo, alipata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali kuanzia kwenye magazeti, Global TV na Global Radio. Baada ya kumaliza ziara yake hiyo fupi ndani ya ofisi hizo, alipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

 

Kabla ya kuanza kuzungumza, Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, alisema: “Global tunatambua mchango na kazi ambayo Jeshi la Polisi Tanzania linafanya, hasa ukiachana na masuala ya ulinzi pia kuna tukio kubwa la Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambao umepita salama, hivyo kwa kutambua mchango huo tumeamua kukupatia Tuzo ya Heshima yenye jina lako.

 

” Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Kamanda Mambosasa alisema: “Ninasema asante kwa tuzo ambayo nimepewa kwani ni kubwa kwangu na inaonyesha kwamba tunashirikiana katika mambo mengi, ninachoweza kusema ni kwamba jamii inabidi itambue polisi siyo adui wa watu bali tunafanya kazi kwa ushirikiano.

 

“Hata akija shabiki wa Yanga ama Simba hata Azam ofisini kwangu mimi nitampokea na kuzungumza naye vizuri tu.”

Comments are closed.