The House of Favourite Newspapers

#GlobalUpdates: Nape Akabidhi Rasmi Ofisi kwa Waziri Mwakyembe

ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye leo amemkabidhi rasmi ofisi waziri mpya wa wizara hiyo, Dkt. Harrison George Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, aliteuliwa Alhamisi iliyopita na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkr. John Pombe Magufuli kuchukua nafasi ya Nape Nnauye wakati nafasi ya Mwakyembe ikichukuliwa na Prof. Palamagamba Kabudi.

 

Comments are closed.